Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi Niger waua magaidi 20 mpakani mwa Nigeria

Niger Niger Wanajeshi Niger yaua magaidi 20 mpakani mwa Nigeria

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Niger limesema kuwa wiki iliyopita liliua magaidi wasiopungua 20 wa kundi la Boko Haram na kuwtaia nguvuni washukiwa wengine 83 wa kundi hilo katika operesheni waliyofanya kwenye mpaka wa nchi hiyo na Nigeria.

Taarifa ya operesheni za kijeshi za jeshila Nigeria katika eneo la Diffa (kusini-mashariki mwa nchi hiyo zimeeleza kuwa, operesheni hiyo ya jeshi la Niger ya anga na ardhini ililenga kuvidhoofisha vituo vya kundi kigaidi la ISWAP la Magharibi mwa Afrika.

Kundi hilo lilijitenga na kundi la Boko Haram na kuasisi kambi zake katika msitu wa Matari nchini Nigeria; ambapo kundi hilo huratibu na kupanga hujuma mashambulizi dhidi ya miji na maeneo ya kijeshi huko Niger.

Taarifa ya jeshi la Niger imeongeza kuwa, magaidi wa ISWAP wasiopungua 20 wameangamizwa na kwamba limewatia mbaroni wshukiwa 83 wa kundi la kigaidi la Boko Haram na kuwakabidhi kwa maafisa husika wa Nigeria.

Kambi tatu za adui", bohari za vifaa, na pikipiki ziliharibiwa katika oparesheni hiyo ya jeshi la Niger na silaha kadhaa zilinaswa. Jeshi la Niger liliendesha oparesheni hiyo kuanzia tarehe 13 mwezi huu hadi tarehe 19 kwa kushirikiana na askari jeshi kadhaa kutoka Niger, NIgeria, Chad na Cameroon.

Wakati huo huo jeshi la Niger limedai kuwa limewatia mbaroni na kuwakabidhi kwa mamlaka husika ya nchi hiyo jumla ya watu 1,121 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram, wakiwemo wanawake na watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live