Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi Niger wagoma kusalimu amri

Kiongozi Wa Mapinduzi Ya Niger Jenerali Tchiani Aahidi Kukabidhi Madaraka Wanajeshi Niger wagoma kusalimu amri

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa kijeshi wa Niger wameidhinisha vikosi vya Mali na Burkina Faso kuingia katika ardhi yake endapo nchi hiyo itashambuliwa.

Taarifa hiyo ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo tatu inaashiria kwamba viongozi wa mapinduzi wa Niger wanapanga kuendelea kutosalimu amri mbele ya mashinikizo la kikanda na kiimataifa ya kuachia madaraka.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hizo tatu walikutana mjini Niamey jana ili kujadili ushirikiano zaidi wa kiusalama na masuala mengine. Burkina Faso na Mali zimekariri msimamo wao wa kukataa uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya Niger ukiutaja kama tangazo la vita.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imekuwa ikijaribu kufanya majadiliano na viongozi wa mapinduzi lakini imeonya kwamba, iko tayari kupeleka wanajeshi nchini humo kwa lengo la kurejesha utulivu endapo juhudi za diplomasia zitashindwa kuzaa matunda. Baraza la Mapinduzi Niger

Hayo yanajiri katika hali ambayo, ECOWAS imekataa pendekezo la utawala wa kijeshi wa Niger la kufanya uchaguzi ndani ya miaka mitatu, na kuzidisha mzozo wa kisiasa ambao unaweza kusababisha uingiliaji wa kijeshi, iwapo hakuna makubaliano yataafikiwa kufuatia mapinduzi ya mwezi Julai.

Kiongozi wa mapinduzi ya Niger ameahidi kulirudisha taifa hilo la Afrika Magharibi katika utawala wa kiraia ndani ya miaka mitatu. Jenerali Abdourahamane Tchiani alitoa tangazo hilo baada ya kukutana na wapatanishi kutoka jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS katika mji mkuu, Niamey.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live