Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi Gabon watangaza kuongoza nchi, wafunga mipaka

Gabon Gabonn Gabonnn.png Wanajeshi Gabon watangaza kuongoza nchi, wafunga mipaka

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: mwanachidigital

Maofisa wa Jeshi la Gabon wametangaza kuiongoza nchi hiyo katika kituo cha televisheni cha Taifa hilo, ikiwa ni siku chache tangu Uchaguzi Mkuu ufanyike.

Pia wamesema wanafuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi, ambapo Rais Ali Bongo alitangazwa mshindi.

Tume ya uchaguzi ilisema Bongo alishinda chini ya thuluthi mbili ya kura katika uchaguzi ambao upinzani ulidai kuwa ulikuwa wa udanganyifu.

Kupinduliwa kwa bongo kunatamatisha uongozi wa familia yake iliyodumu kwa miaka 53 madarakani nchini Gabon.

Wanajeshi 12 walionekana kwenye televisheni siku ya Jumatano, wakitangaza suala hilo huku pia wakitangaza kufunga mipaka ya nchi hiyo.

"Tumeamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo,"alisema mmoja wa wanajeshi hao.

Ofisa huyo wa jeshi aliongeza kuwa sababu nyingine ni; "utawala usiowajibika, usiotabirika na kusababisha kuzorota kwa uwiano wa kijamii ambao unahatarisha nchi katika machafuko".

Chanzo: mwanachidigital