Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi 8 wa UN mbaroni unyanyasaji wa kingono

Vikosi Munucos DRC Wanajeshi 8 wa UN mbaroni unyanyasaji wa kingono

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Beni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) ulitangaza jana Jumatano kwamba umechukua "hatua kali" dhidi ya walinda amani wanaoshukiwa kwa "makosa makubwa".

Kwa mujibu wa nyaraka za ndani za MONUSCO zilizovuja, askari hao 8 wa MONUSCO, walikamatwa Oktoba 1, na afisa mmoja alisimamishwa kazi tarehe 8 kupisha uchunguzi wa ndani baada ya kuenea kwa madai ya unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji dhidi ya watu kwenye mji wa Beni mkoani Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Taarifa hiyo imesema kuwa askari wote 8 waliokamatwa ni wa kikosi cha Afrika Kusini wanaohudumu chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifaو na kwamba wanahusika katika ukiukaji wa taratibu na sheria za Umoja wa Mataifa dhidi ya unyanyasaji wa kingono.

Tangu mwezi Mei, Rais wa Congo DR, Felix Tshisekedi amekuwa akitoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, kupeleka wanajeshi nchini humo kulisaidia jeshi la Congo katika kukabiliana na waasi wa M23, ambao wameteka maeneo makubwa ya Kaskazini.

Wakati huo huo Serikali ya DRC imekuwa ikitoa wito wa kuondoka kikosi cha Umoja wa Mataifa kuanzia mwezi Disemba, ikikishutumu kwamba kimeshindwa kukomesha ghasia za makundi yenye silaha katika kipindi chote cha miaka 25 ya kuwepo kwake nchini Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live