Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi 12 wa Niger wauawa katika shambulizi la wanamgambo

Wanajeshi Niger Wanajeshi 12 wa Niger wauawa katika shambulizi la wanamgambo

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ulinzi wa Niger ametangaza habari ya kuuawa wanajeshi wasiopungua 12 wa nchi hiyo katika shambulizi la kundi la wanamgambo kusini magharibi mwa nchi.

Salifou Mody amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Anadolu na kuongeza kuwa, wanajeshi saba waliuawa katika shambulizi la kigaidi la jana Alkhamisi katika eneo la Kandadji, yapata kilomita 190 kutoka mji mkuu Niamey.

Ameongeza kuwa, wanajeshi wengine watano waliuawa katika ajali ya barabarani, walipokuwa wanajaribu kujibu shambulizi hilo la wanamgambo katika eneo hilo lililoko katika mpaka wa Niger, Mali na Burkina Faso.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, wanajeshi wengine 12 wa Niger waliuawa katika shambulizi jingine la kuvizia na watu wanaoshukiwa kuwa magaidi katika kijiji kimoja kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Shambulizi hilo lilikuja siku chache baada ya wanajeshi wengine 17 kuuawa wakati watu wenye silaha walipovizia kikosi cha jeshi karibu na mji wa Koutougou katika eneo la Tillaberi karibu na mpaka na Burkina Faso. Waniger katika maandamano ya kutaka kuondoka nchini humo vikosi vya Ufaransa

Mashambulizi hayo yanajiri licha ya Ufaransa kuwa na takriban wanajeshi 1,500 nchini Niger, wengi wao wakiwa katika kambi ya kijeshi ya nchi hiyo iliyoko Niamey. Hata hivyo Jumapili iliyopita, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa nchi yake itapanga kuondoka kwa wanajeshi wake kutoka Niger katika wiki au miezi ijayo, na kuongeza kuwa askari wote watakuwa wamerejea nyumbani hadi mwisho wa 2023.

Baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi ya Niger (CNSP) hivi karibuni lilisema kuwepo kwa vikosi vya Ufaransa nchini Niger hakukubaliki, na kupokea kwa mikono miwili tangazo la Ufaransa la kuondoa askari wake katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live