Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi 10 wajeruhiwa na magaidi kadhaa Niger

Watu 85 Wauawa Katika Shambulio La Anga Nigeria Wanajeshi 10 wajeruhiwa na magaidi kadhaa Niger

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Niger, wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wapiganaji "kadhaa" kutoka kundi la wanajihadi la Boko Haram waliuawa siku ya Jumanne wakati wa mapigano katika eneo la Niger la Ziwa Chad (kusini-mashariki). Hii imebainishwa katika taarifa ya serikali iliyotolewa Jumanne jioni.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Niger, wanajeshi hao kumi walijeruhiwa katika mapigano na wapiganaji wa Boko Haram ambao walitekeleza shamblio siku ya Jumanne mwendo wa saa 7:50 usiku dhidi ya kikosi maalum cha kuingilia kati kilichokuwa kwenye uwanja wa ndege wa N'Guigmi, mji ulio katika mkoa wa Diffa karibu na Nigeria.

Baada ya mapigano yaliyodumu "takriban dakika ishirini", wanajeshi waliweka "upinzani mkali" na "kuwatimuwa" washambuliaji "kuelekea mwambao wa Ziwa Chad", kati ya Niger, Nigeria na Chad, inabainisha taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi iliyotolewa siku ya Jumanne jioni.

Msako ulioanzishwa kwa ulifanya iwezekane kuwapata washambuliaji “waliokuwa wakijaribu kutorioka wakitumia mitumbwi kumi” kwenye Ziwa Chad.

"Magaidi kadhaa" "waliangamizwa (kuuawa)" katika mashambulizi ya anga ya na "mitumbwi yote iliharibiwa," taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi imebainisha.

Haya ni matukio ya mabaya zaidi yaliyoripotiwa kati ya jeshi na wanajihadi baada ya miezi kadhaa ya utulivu katika eneo hili, linalo kumbwa tangu mwaka 2015 na mashambulizi ya kundi la Boko Haram lililoanzishwa nchini Nigeria, na Islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP), tawi lake lililojitenga na kundi hili.

Mojawapo ya matukio mabaya yalitokea mwezi Juni 2023: askari saba waliuawa katika mlipuko wa bomu la ardhini huko Chétima Wangou, karibu na mji wa Diffa, mji mkuu wa mkoa.

Eneo hili lina maelfu ya wakimbizi wa ndani na wakimbizi wa Nigeria ambao wanategemea mashirika ya kibinadamu na wakazi wa eneo hilo, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na mavuno duni yaliyosababishwa na ukame, kulingana na mamlaka za kikanda.

Niger, inayoongozwa na utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya Julai 26, 2023, pia inakabiliwa na vitendo vya mauaji vya makundi ya wanajihadi yanayohusishwa na Al Qaeda na Islamic State katika Sahara Kuu (EIGS), magharibi mwa nchi, karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live