Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi 10,000 kusaidia uokoaji adha ya mafuriko

Mafuriko South Wanajeshi 10,000 kusaidia uokoaji adha ya mafuriko

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Afrika Kusini linasema linawapeleka wanajeshi zaidi ya 10,000 kusaidia katika shuguli za misaada na uokoaji kufuatia mafuriko mabaya yaliyosomba baadhi ya maeneo ya jimbo la KwaZulu-Natal wiki iliyopita.

Zaidi ya watu 440 wamefariki, na msako unaendelea kwa ajili ya kuwasaka watu wengine 63 ambao bado hawajulikani walipo.

Baadhi yao walisombwa na mito iliyofurika na maporomoko ya ardhi.

Serikali imeitakanga KwaZulu-Natal eneo la mkasa.

Maafisa wameyaelezea mafuriko kama mabaya kuwahi kuilikumba jimbo hilo.

Waziri mkuu wa KwaZulu-Natal Sihle Zikalala amesema kuwa karibu nyumba 4,000 ziliangamia huku zaidi ya 8,000 zikiharibiwa, nyingi kati yake katika mji wa mwambao wa Durban na maeneo yanayouzingira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live