Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaigeria waliokuwa wakienda hija Saudia walazimika kurudi nyumbani

Wanaigeria Waliokuwa Wakienda Hija Saudia Walazimika Kurudi Nyumbani Wanaigeria waliokuwa wakienda hija Saudia walazimika kurudi nyumbani

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Zaidi ya Wanigeria 170 waliokuwa kwenye ndege kuelekea Saudi Arabia walirudishwa nyuma siku ya Jumatatu baada ya mamlaka ya Saudia kuripotiwa kufutilia mbali viza zao, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti.

Ripoti zinasema kuwa abiria 264, ambao walikuwa wameondoka katika miji ya Lagos na Kano ya Nigeria, walipokea viza na kufanyiwa uchunguzi mkali kabla ya kupanda ndege.

Hata hivyo, viza zao zote ziliripotiwa kufutwa wakiwa angani.

Walipofika, mamlaka ya Saudia iliripotiwa kukataa kuwaruhusu kuingia na kuamuru shirika la ndege la Air Peace la Nigeria kuwarejesha nyumbani Nigeria, ripoti zinaongeza.

Mamlaka ya Saudia haijazungumzia suala hilo.

Abiria walioathiriwa wameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba walishangaa kusikia kuhusu kukataliwa kwa viza walipotua kwani walikuwa wamekidhi mahitaji yote ya kuingia katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia inasemekana hatimaye iliruhusu kuingia kwa abiria 87 baada ya balozi wa Nigeria nchini humo kuingilia kati lakini 177 walirejeshwa Nigeria Jumatatu usiku.

Ripoti za vyombo vya habari vya Nigeria zinasema wengi wa abiria hao walikuwa wamesafiri hadi Saudi Arabia kutekeleza ibada ndogo ya Hija (Umrah), kuhiji katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Makka.

Chanzo: Radio Jambo