Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaigeria waandamana kuipinga ECOWAS dhidi ya Niger

Ecowas Ecowas Ecowasss.jpeg Wanaigeria waandamana kuipinga ECOWAS dhidi ya Niger

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya watu nchini Nigeria wamefanya maandamano wakipinga uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Kanda ya Afrika Magharibi, (ECOWAS) nchini Niger.

Shirika la Habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa, waandamanaji katika jimbo la Kano nchini Nigeria, waliokuwa wamebeba bendera ya Niger, walieleza upinzani wao kwa msimamo wa ECOWAS kuhusu uwezekano wa kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nchi jirani ya Niger.

Waandamanaji hao pia walitoa kauli mbiu dhidi ya ECOWAS na serikali ya Nigeria, wakisema "Niger ni jirani", "vita dhidi ya Niger ni vya kidhalimu", na kwamba "mashambulizi hayo yanachochewa na nchi za Magharibi".

Baada ya makataa yake kupuuzwa na waliopanga mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilitoa taarifa Alkhamisi iliyopita ikitilia mkazo nia yake ya kubakisha mezani machaguo yote ya kutatua mzozo wa Niger, huku Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, akifichua kwamba kundi hilo limetoa mwanga wa kijani kwa operesheni ya kijeshi ambayo "itaanza haraka iwezekanavyo."

Taarifa hiyo ililaani "mapinduzi ya kijeshi nchini Niger na kuendelea kukamatwa kwa Rais Mohamed Bazoum," na kusema kwamba "machaguo yote yako mezani kuhusu Niger, ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu kama suluhisho la mwisho."

Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa wakati wa kuhitimisha mkutano wao wa kilele katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, viongozi wa ECOWAS walisisitiza uungaji mkono wao kwa suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro wa Niger.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live