Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wenye rekodi za nidhamu mbovu kutojiunga na vyuo Kenya

0fdde18d94424387 Wanafunzi wenye rekodi za nidhamu mbovu kutojiunga na vyuo Kenya

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya Elimu nchini Kenya imetangaza kwamba wanafunzi watakaopatikana na rekodi ya utovu wa nidhamu hawatapata nafasi ya kuendeleza masomo yao katika taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu ya umma.

Katibu Mkuu wa elimu katika vyuo vikuu na utafiti Simon Nabukwesi amesema serikali kwa sasa inakabiliana na mikasa ya moto ambayo inaendelea kuripotiwa katika vyule.

Akizungumza akiwa katika chuo kikuu cha Kibabii, Katibu Mkuu wa elimu katika vyuo vikuu na utafiti Simon Nabukwesi alisema wanafunzi wanaojihusisha na visa vya uteketezaji vyule na uharibifu wa mali hawakubaliwa katika vyuo vikuu vya umma kwa ajili ya utovu wa nidhamu.

Nabukwesi alisema kwa sasa serikali inakabiliana na visa vya wanafunzi kuchoma vyule ambavyo vimekithiri nchini.

"Mtu yeyote anayechoma jumba, liwe lao au la kwa mara nyingi hupata laana na huwa hafaidiki na chochote kutoka kwa jamii hata awe na elimu ya juu ya aina gani. Naomba kama idara ya upelelezi ina majina ya wale wanafunzi ambao wanajihusisha na uchomaji vyule, tuyatumie katika wizara ya elimu ili wasiwate nafasi katika taasisi na vyuo vikuu kwa sababu wataendeleza mwenendo huo," Nabukwesi alisema.

Nabukwesi pia alisema serikali iko katika harakati ya kufanya ukaguzi wa utendakazi kwa walimu wakuu wa shule zote nchini haswa za upili.

Serikali pia iliamuru shule zote zifungwe kwa likizo fupi kuanzia Ijumaa, Novemba 19 mwaka huu.

Chama cha walimu wa shule za upili, KUPPET kimeitaka wizara ya afya irejeshe shuleni adabu kali kwa wanafunzi angalau visa vya uchomaji shule vitapungua.

Shule kadhaa ikiwemo ya Kakamega zimeteketezwa chini ya muda wa wiki mbili zilizopita, baadhi ya wanafunzi wanazuiliwa kufuatia mikasa ya moto shuleni.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke