Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wengine wa Sudan wamewasili Rwanda kuendelea na masomo

Wanafunzi Wengine Wa Sudan Wamewasili Rwanda Kuendelea Na Masomo Wanafunzi wengine wa Sudan wamewasili Rwanda kuendelea na masomo

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kundi la wanafunzi kutoka Sudan lilipokelewa siku ya Jumanne katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Rwanda katika mji wa Huye, ambapo wanakwenda kuendelea na masomo yao ya udaktari.

Wanafunzi hawa waliofika Rwanda walikuwa waanze mwaka wa kwanza wa utabibu katika Chuo Kikuu kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Teknolojia.

Wanafunzi hawa walifika Rwanda kuendelea na masomo baada ya chuo kikuu chao kushambuliwa na wanamgambo.

Hili ni kundi la pili la wanafunzi hao kuwasili Rwanda baada ya kundi la kwanza kuwasili nchini humo mwanzoni mwa mwezi wa nane.

Kulingana na tangazo la televisheni ya taifa, kundi la wanafunzi 200 lilipokelewa siku ya Jumanne katika Chuo Kikuu cha Rwanda, Kitivo chake cha Tiba kilichopo katika mji wa Huye (katika jimbo la kusini).

Ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Teknolojia (UMST).Chuo Kikuu hiki tayari kimekaliwa na wapiganaji ambao waligeuza kuwa msingi kama ilivyothibitishwa na viongozi wake.

Tangu mwezi wa nne, nchi ya Sudan imekuwa kwenye vita kati ya majenerali wawili: Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) na Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti, mkuu wa kitengo cha kijeshi kinachojulikana. kama Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Kwa upande wa Rwanda, Chuo Kikuu cha Kitaifa kinasema kwamba kimekubali kuwapokea wanafunzi hao kama sehemu ya juhudi za kutoa msaada, lakini haitabadilisha chochote kuhusu mpango wao wa masomo.

Chanzo: Bbc