Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi warejea shule Burundi leo, Uganda haifungui shule bija chanjo

Buruni Wanafunzi warejea shule Burundi leo, Uganda haifungui shule bija chanjo

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Burundi yafungua shule zote huku Uganda ikisisitiza chanjo kwanza.

Serikali ya Burundi imezingua shule zote nchini humo kuanzia leo September 13, 2021 ikiwa ni takribani miezi mitatu tangu ilipoagiza kufungwa shule ili kudhibiti kasi ya maambukizi nchini humo.

Wizara ya Afya imeagiza ukaguzi, kuchukuliwa tahadhari zote za kujikinga na COVID-19 pamoja na vipimo kwa wanafunzi wote wanaoanza kutejea mashuleni kuanzia leo.

"Vipimo ni lazima kwa wanafunzi wote wa nje ya shule na wale wanaokaa bweni, wengine wataendelea na vipimo vya hiari," amesema Jean Bosco Girukwishaka ambaye ni Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Burundi.

Upimaji wa jumla kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazi wa mashule ulianza rasmi Ijumaa September 10, 2021 na utaendelea mpaka Jumanne Sept, 14, 2021.

"Kwenye wiki ya kwanza ya September 2021, visa vya COVID-19 viliongezeka hasa kwenye jiji la Bujumbura na miji mingine ya Burundi, kutochukua tahadhari imetajwa kuwa sababu kuu ya kusambaa kwa kasi kwa maambukizi ya Corona" inasomeka taarifa ya Wizara ya Afya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kuhusu COVID-19 iliyotolewa September 6, 2021, wastani wa maambuki ya kila siku yamebaki kuwa watu 154 tangu July 21, 2021 ambapo ilitolewa taarifa ya visa vingi zaidi vya Corona.

Wakati hali ikiwa hivyo, Nchi ya Uganda bado imezifunga shule zake mpaka sasa, pamoja na maagizo ya viongozi wa serikali kuagiza utoaji chanjo nchini humo bado kumekua na kasi ndogo ya walimu na wafanyakazi wa shule kujitokeza kupata chanjo. Hivi karibuni, mke wa Rais, mama Janet Museven alisisitiza kuwa shule zitafunguliwa endapo tu wafanyakazi watakua wamechanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live