Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi waliotekwa nyara waachiliwa huru Nigeria

AP24084242488722 Wanafunzi waliotekwa nyara waachiliwa huru Nigeria

Sun, 24 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wanafunzi 280 waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa mji wa Kuriga nchini Nigeria mapema mwezi huu wameachiliwa huru “bila madhara”, maafisa wamesema.

Gavana wa jimbo la Kaduna Uba Sani hakutoa taarifa zaidi kuhusu kuachiliwa kwa wanafunzi hao, ikiwa ni siku kadhaa kabla ya makataa ya kulipa kikombozi iliyotolewa na watekaji kufika.

Wanafunzi hao wenye umri wa kati ya miaka minane hadi 15, na mwalimu mmoja walitekwa Machi 7.

Makundi ya watekaji, yameteka maelfu ya watu miaka ya hivi karibuni, hasa katika eneo la kaskazini-magharibi.

Wakati huu, watekaji walidai kikombozi cha dola 690,000. Serikali ilisema haotolipa kikombozi chochote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live