Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi waliodai ni yatima wafutiwa mikopo

Ugggg.png Wanafunzi wachuo

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Uganda imewafutia mikopo Wanafunzi 47, baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika taarifa za wanafunzi hao.

Wanafunzi hao walitumia udanganyifu kwa kudai kuwa ni yatima, wanalelewa na mzazi mmoja na wengine 10 kati yao kudai kuwa ni walemavu ili wapate urahisi wa kupata mkopo huo wa Elimu ya juu.

Aidha, Bodi ya mikopo kwa Wanafunzi nchini humo imeamuru kuwa wanafunzi hao waanze kujilipia ada pamoja na kurejesha pesa ya Serikali amabayo wamekwisha tumia.

Bodi ya mikopo kwa Wanafunzi nchini humo hupendekeza kuwapa kipaumbele wanafunzi wenye uhitaji zaidi ili kuwasaidia kufikia malengo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live