Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wakwama masomo mzozo DRC na Rwanda

Mzozo Rwanda Shuleeee.png Wanafunzi wakwama masomo mzozo DRC na Rwanda

Mon, 27 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wa Rwanda wanaosoma mjini Goma-DRC wanakabiliwa na vitisho vya usalama kutokana na mzozo uliopo kati ya nchi hizo mbili jirani.

Hali bado si shwari mpakani na hii inazua wasiwasi miongoni mwa baadhi ya wazazi katika mji wa Rubavu ambao watoto wao wanaosomea nchini DRC , wakisema kuna hatari ya wao kulengwa kutokana na jinsi walivyo.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana akiwa mjini Rubavu amezungumza na baadhi ya wanafunzi na wazazi ili kujua jinsi mivutano na machafuko hayo yanavyoathiri elimu yao.

Alianza kwa kutembelea mtaa wa kifahari uliopewa jina la RCD mjini Rubavu wanamoishi raia wengi.

Anasema kwamba baadhi ya wanafunzi raia wa Rwanda wanaoishi katika eneo hilo walishindwa kurejea katika shule zao mjini Goma.

Wanafunzi hao ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwa sababu za usalama wao walielezea masaibu yao:

Mmoja wao ananukuliwa akisema kwamba wale walio na familia zao mjini Goma walikubaliwa kusalia huku wengine walio na familia nchini Rwanda wakitakiwa kurudi nchini Rwanda mara moja.

Mama mmoja ambaye pia hakutaka jina lake litajwe kwa sababu ya usalama wa watoto wake 4 wanaosomea mjini Goma anasema kwamba awali watoto wake wamekuwa wakisomea mjini Goma na kurudi nchini Rwanda bila tatizo lolote lakini sasa ni mmoja ya wazazi ambao wamekuwa na shaka.

“Watoto wangu wanasomea Goma huku wakirudia nchini Rwanda, mwanzo hakukuwa na tatizo lakini kwa sasa kutona na hali ilivyo tuna mashaka sana. siku ya kwanza ya maandamano nilipata wasi wasi mkubwa-mtoto wangu alichukua boda boda toka shuleni ili kumfikisha mpakani walipofika katikati ya njia alipomwambia mwendesha boda boda kuwa anaelekea kwenye mpaka wa Rwanda akamuacha hapo kwa kumwambia :’kumbe wewe ni Mnyarwanda’ si unaona ni shida?’

Chanzo: www.tanzaniaweb.live