Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wakamatwa, wadaiwa kutoa vitisho vya kigaidi

Mbaroni (1) Wanafunzi wakamatwa, wadaiwa kutoa vitisho vya kigaidi

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza, Shule ya Sekondari St Charles Lwanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda baada ya kukamatwa wilaya za Bushenyi na Sheema kwa madai ya kutoa vitisho vya kigaidi toka kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), kwa shule tatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa nchi hiyo, wanafunzi hao walikamatwa kwa madai ya kutishia mashambulizi dhidi ya shule ya Sekondari ya St Charles Lwanga na shule nyingine mbili za Kasese (Shule ya Msingi St Andrews na Shule ya Msingi Kibingo).

Mtandao wa Monitor umeandika kuwa, wawili hao walitoa vitisho hivyo kupitia barua, huku wakificha yao na kuitupa bila utambulisho wowote kwenye lango la moja ya vyumba vya madarasa.

Polisi walisema mnamo Julai 5, 2023, uongozi wa shule ulikumbana na barua hiyo na baada ya uchunguzi wa kina ilibainika kuwa barua hiyo isiyojulikana iliandikwa na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 akisaidiwa na mwenzake mwenye umri wa miaka 17.

Walidai walitaka kuwatisha wasimamizi wa shule kwa kuwaadhibu baada ya kiongozi wa bweni lao kuwasilisha ripoti ya utovu wa nidhamu dhidi yao.

Kulingana na msemaji wa Polisi, SCP Fred Enanga, wanafunzi hao wawili walikiri kuandika barua hiyo ambayo ilikuwa na vitisho vya ugaidi dhidi ya shule tatu.

"Wanafunzi wote wawili walikiri kuwa waliandika barua hiyo bila majina. Kikosi kazi chetu pia kilipata kitabu cha mazoezi ambayo waliyachora kwenye barua hiyo. Itawasilishwa, pamoja na vielelezo vyao vya maandishi, kwa mtaalamu wa uandishi kwa uchambuzi,” Enanga alisema na kuongeza;

“Tungependa kuwaonya wanafunzi kwamba kutoa vitisho vya vurugu au kushambulia au kutumia silaha za moto si mzaha, bali ni kitendo cha uhalifu. Wanafunzi hao wawili watafikishwa mahakamani kwa kutishia kufanya vurugu na pengine wanaweza kushikiliwa kwenye gereza la watoto.”

Kukamatwa kwao kumekuja siku chache baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa ADF kuvamia Shule ya Sekondari ya Lhubiriha iliyoko Wilaya ya Kasese magharibi mwa Uganda na kuwaua zaidi ya watu 40 wengi wao wakiwa wanafunzi kabla ya kuwateka nyara wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live