Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wachoma bweni kisa Man UTD na Liverpool

Screen Shot 2021 10 27 At 10.png Wanafunzi wachoma bweni kisa Man UTD na Liverpool

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: Kenya 24

Wavulana wanne wa shule nchini Kenya wanashikiliwa katika mahabusu ya polisi kwa kulichoma moto bweni la shule yao, baada ya kuripotiwa kunyimwa ruhusu ya kutazama mechi kati ya Liverpool na Manchester United, umeripoti wavuti wa Daily Nation nchini humo.

Lilimnukuu mkuu wa polisi wa eneo akisema kuwa wanafunzi hao walikuwa miongoni mwa wengine 14 wanohojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Wanafunzi hao wanne wanaosoma katika shule ya sekondari yaDr Krapf iliyopo katika eneo la pwani ya Kenya la Kilifi watashitakiwa kwa kosa la kuchoma moto kwa makusudi bweni siku ya Jumatano.

Wanafunzi shuleni wanaruhusiwa tu kutazama televisheni Jumamosi, alisema kamanda wa polisi wa Rabai Fredrick Abuga katika mazungumzo na wavuti wa Daily Nation.

Shule yao kwa sasa imefungwa kufuatia tukio hilo.

Liverpool iliiadhibu timu ya Manchester United kwa kuichapa mabao 5-0 katika uwanjawao wa Old Trafford.

Chanzo: Kenya 24