Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi sita UDSM watikisa shindano la TEHAMA Huawei, sasa kuiwakilisha Afrika duniani

730e21b2acb0f16f62e1e56375877586 Wanafunzi sita UDSM watikisa shindano la TEHAMA Huawei, sasa kuiwakilisha Afrika duniani

Sat, 14 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wanafunzi sita wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefuzu kushiriki shindano la Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) duniani yanayoandaliwa na Huawei baada ya kufanya vizuri katika ukanda wa Jangwa la Sahara ya Huawei.

Hayo yamefahamika baada ya kuanyika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi ilifanyika kwa njia ya mtandaoni Oktoba 29, 2020.

Lengo la Huawei kuandaa shindano hilo ni kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji katika tasnia ya TEHAMA kuonyesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, kuhimiza utafiti wa TEHAMA na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Timu 13 zilizoshinda zinatoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Lesotho, Mauritius na Zambia.

Washindi hao kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara watapambana kuonesha umahiri wa matumizi ya TEHAMA na wapinzani wao kutoka mabara mengine ikiwemo Amerika ya Kaskazini, mwezi huu.

Miongoni mwa timu zilizopewa tuzo kwenye hafla hiyo ni

Timu 10 zilizoshiriki kuwania katika kipengele cha Network Track zikiwemo timu kutoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na Lesotho zilipewa tuzo.

Nyingine zilizopewa tuzo katika kipengele cha Cloud Track zinatoka Nigeria, Mauritius na Zambia.

Wanafunzi wa Kitanzania tisa walishiriki shindano hilo ambao kwa ujumla waliunda timu tatu ambapo mbili kati ya hizo kufika fainali kushika nafasi ya kwanza kati ya 40 huku timu moja ikichomoza katika nafasi ya nne.

Timu hizo zimeundwa na wanafunzi wa ndaki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Washindi wa nafasi ya kwanza ni Mpoki Mwaisela, Hongo Kelvin na Henry Kihanga na washindi wa pili ni Aghatus Biro, John Lazaro na Elisante Akaro.

Hafla hiyo ya utoaji tuzo imeashiria miaka mitano mfululizo ya kushiriki kikamilifu

Shindano la TEHAMA la Huawei kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara limefanyika kwa miaka mitano mfululizo huku likivutia wanafunzi 50,000 kutoka nchi 14 za Afrika.

“Fursa za kukuza ujuzi zinazotolewa na Kampuni ya Huawei ni muhimu sana ambapo sasa tunahitaji utaalam mwingi barani Afrika kuliko wakati wowote kabla, hasa ukizingatia changamoto zilizoletwa na janga la COVID-19 kwenye mfumo wetu wa elimu,” Dk Kisaka, Mkuu wa Ndaki COICT ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema.

Shindano la TEHAMA la Huawei ni moja ya tukio kubwa la aina yake ambalo linawaleta pamoja wanafunzi pamoja kwa lengo la kuonesha ujuzi wao katika sekta ya teknolojia kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Zambia, Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

Chanzo: habarileo.co.tz