Nchini Afrika Kusini, kitengo cha Elimu kimewataka wanafunzi wote wa eneo la KwaZulu-Natal Agosti 30, siku ya Jumanne kuvaa mavazi yanayoendana na mfalme mpya wa Wazulu Misuzulu ka Zwelithini Zulu.
Kitengo hicho cha elimu cha jimbo la KwaZulu-Natal kimesema mfalme huyo mpya mwenye Umri wa miaka 48, atafanyiwa sherehe za kumuadhimisha Agosti 30.
Kitengo hicho cha Elimu kinawashauri walimu wote na wafanyakazi kuvaa nguo za kitamaduni siku hiyo ya kihistoria ya kumuenzi mfalme wao mpya.
Mavazi nchini Afrika Kusini ni swala ambalo linapewa kipaumbele zaidi hasa katika asili ya kizulu na mara nyingi ni mavazi yanayokuwa na ngozi za wanyama na zende muonekano wa rangi nyingi.
Misuzulu ka Zwelithini alitawazwa katika Sherehe za kitamaduni siku ya Jumamosi ingawa baadhi ya viongozi wa Kimila walidai kuwa hakuwa anafaa kushika wadhifa huo.
.