Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi Kenya warejea shuleni leo, baada ya kukaa nyumbani miezi 9

1e618a759cd24d42f3b6cf8cd770efb3 Wanafunzi Kenya warejea shuleni leo, baada ya kukaa nyumbani miezi 9

Sun, 10 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SHULE nchini Kenya zimefunguliwa rasmi leo baada ya kufungwa kwa miezi tisa kufuatia mlipuko wa Covid-19.

Aidha Waziri wa Elimu nchini humo, George Magoha ameendelea kukagua jinsi shule zinavyofunguliwa.

Hata hivyo, baadhi ya wazazi wa wanafunzi wamelalamika watoto wao kukosa nafasi katika shule kutokana na nafasi kujaa kwa mujibu wa maelekezo ya kikomo cha idadi ya wanafunzi katika shule husika ili kudhibiti msongamano.

Moja ya sababu zilizotajwa kupelekea changamoto ya kukosekana kwa nafasi ni baadhi ya wamiliki binafsi kuzifunga shule zao kutokana na kushindwa kuziendesha kufuatia athari za Covid-19, hivyo wazazi kulazimika kuzunguka kuwatafutia watoto wao nafasi katika shule nyingine.

Chanzo: habarileo.co.tz