Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 60,000 waliofeli mitihani kurudia madarasa Rwanda

A Candidate Sitsrrrrr Wanafunzi 60,000 waliofeli mitihani kurudia madarasa Rwanda

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wanafunzi 60,000 waliofeli mitihani ya kitaifa nchini Rwanda wanatarajia kurudia madarasa hayo kufuatia mpango mpya wa Serikali wa kukuza ufaulu kwa wanafunzi.

Lengo la hatua hiyo ni kutaka kuboresha mfumo wa elimu pamoja na kuongeza ufaulu wa masomo kwa wanafunzi wote nchini humo.

Katika matokeo yaliyotolewa tarehe 04, Oktoba 2021, na Wizara ya Elimu imeonesha kuwa jumla ya wanafunzi 44,000 sawa na asilimia 17 katika shule za msingi na wanafunzi 16,000 sawa asilimia 13.6 kwa shule za sekondari wamefanya vibaya kwenye mitihani na watatakiwa kurudia madarasa hayo.

Jumla ya wanafunzi 251,906 walisajiliwa kufanya mtihani wa shule za msingi, na wanafunzi 121,626 kwa shule za sekondari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live