Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 20 wa chekechea wateketea kwa moto Niger

Thumbs B C 7682179bf1c86cc3f630b6671bec9b8c 660x400.jpeg Wanafunzi 20 wa chekechea wateketea kwa moto Niger

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Watoto 20 wamefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea Shule moja katika Mji Mkuu wa Niger, Niamey. Imeelezwa, moto ulianza wakati watoto wakiwa kwenye vipindi na wengi wao walikuwa madarasa yaliyoezekwa kwa makuti.

Kwa mujibu wa taarifa, moto ulizuia lango la Shule na kupelekea Wanafunzi wengi kulazimika kujiokoa kwa kuruka ukuta. Wengi walioshindwa kufanya hivyo walikuwa Wanafunzi wa chekechea.

Chanzo cha moto huo ambao umeteketeza madarasa 28 yaliyoezekwa kwa makuti na kuharibu mengine 30 yaliyojengwa kwa matofali bado hakijafahamika.

OFISINI KWA RAIS SAMIA IKULU, AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS MPANGO WAFANYA MAZUNGUMZO

Chanzo: millardayo.com