Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 17 wafariki kwa mlipuko wa homa ya utindio wa ubongo Nigeria

Wanafunzi 17 Wafariki Kwa Mlipuko Wa Homa Ya Utindio Wa Ubongo Nigeria Wanafunzi 17 wafariki kwa mlipuko wa homa ya utindio wa ubongo Nigeria

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Wanafunzi 17 katika shule tano katika jimbo la Yobe kaskazini-mashariki mwa Nigeria wamefariki baada ya mlipuko wa homa ya uti wa mgongo, mamlaka imethibitisha.

Miongoni mwa waliofariki ni wanafunzi wa shule za msingi na wengine katika shule za upili za bweni, kamishna wa elimu wa serikali, Mohammed Sani-Idris, aliambia BBC.

Jumla ya kesi 473 zinazoshukiwa zimerekodiwa hadi sasa, alisema. Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi ambayo husababisha kuvimba kwa tabaka za nje za ubongo na uti wa mgongo.

Inaweza kuhatarisha maisha isipokuwa kutambuliwa na kutibiwa mapema.

Chanjo ni njia bora ya kuzuia ugonjwa wa utindio wa ubongo.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Nigeria (NCDC) mapema mwakani kilitoa ushauri wa afya ya umma kuhusu ugonjwa huo.

Ilionyesha kuwa msimu wa kiangazi unaweza "kuongeza hatari ya kuambukizwa, hasa maeneo yenye msongamano yasiyo na hewa safi ".

Visa vingi vya ugonjwa huo nchini Nigeria vinaripotiwa katika kile kinachojulikana kama "Maeneo yanayoathiriwa sana," katika majimbo yote 19 katika ya kaskazini.

Chanzo: Bbc