Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 15 wafa kwa kukanyagana Kenya

94423 Wanafunzi+pioc Wanafunzi 15 wafa kwa kukanyagana Kenya

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kakamega, Kenya. Wanafunzi 15 wa Shule ya Msingi, Kakamega nchini Kenya wamefariki dunia baada ya kukanyagana.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kakamega, David Kabena alisema kuwa wanafunzi wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa na 20 kati yao wamepata matibabu na kuruhusiwa.

Kabena alisema baadhi ya wanafunzi wako katika hali mbaya jambo ambalo linaweza kuongezaidadi ya vifo.

Akisimulia tukio hilo Kabena alisema mkanyagano huo ulitokea baada ya king’ola kupigwa kikiashiria hali ya dharura.

“Baada ya king’ola hicho kilizua taharuki na kusabisha wanafunzi kukimbia ovyo huku wengine wakiruka kutaka kujikomboa jambo lilosababisha kukanyagana na baadhi kuanguka,” alisema.

Alisema baadhi yao walianguka kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hilo walipokuwa wakitoka darasani.

Pia Soma

Advertisement
Alisema kuwa baada ya tukio taratibu za kuwapeleka majeruhi katika Hospitali ya Kakamega zilifanywa ili kuwanusuru ambako baaadhi yao walilazwa katika chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU).

Wazazi wamekusanyika hospitalini wakiwa na hofu kuwa inawezekana kuna wanafunzi wengi zaidi wamejeruhiwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz