Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 1,000 wanaaacha masomo kila mwaka kwa Kubeti

Betting 20x1080 Wanafunzi 1,000 wanaaacha masomo kila mwaka kwa Kubeti

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuo Kikuu cha Makerere kimesema takriban Wanafunzi 1,000 wanaacha au kuachishwa Masomo kila mwaka kutokana na kupoteza Fedha za Ada wanazozitumia kwenye Michezo ya Kubashiri maarufu kama 'Kubeti'

Kauli hiyo imetolewa na Profesa Barnabas Nawangwe ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho ambaye amesema Chuo kililazimika kufanya tafiti kujua sababu za Wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo

Amesema; "Uchunguzi wetu umeonesha kuwa kweli watu hao walikuwa wanaacha shule sio kwa sababu walishindwa kulipa ada. Walipata ada kutoka kwa wazazi wao lakini walitaka kuwekeza katika kamari ili kupata faida.”

Aidha kwa mujibu wa takwimu za #DriveResearch Sekta ya Michezo ya Kubashiri (Betting) duniani kote ilikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 235 (zaidi ya Tsh. Trilioni 599.25) mwaka 2022 huku ikiwa na Wacheza kamari takriban Milioni 176. Idadi hiyo inatajwa kuwa itafika Watu Milioni 210 mwaka 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live