Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wana bendi wakamatwa kwa 'kumtusi' Museveni

Wana Bendi Wakamatwa Kwa 'kumtusi' Museveni Wana bendi wakamatwa kwa 'kumtusi' Museveni

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Wanachama wanane wa bendi ya muziki nchini Uganda wamekamatwa kwa kulalamika kwamba hotuba ya rais mwishoni mwa juma ilikuwa ndefu sana, vyombo vya habari vya nchini vimeripoti.

Malalamiko ya mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo yalionekana kuwa ni dharau kwa Rais Yoweri Museveni, ambaye alikuwa akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya harusi ya Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi na mkewe Jacqueline Mbabazi Jumamosi usiku.

Wanachama wa bendi ya Crane Performers walikuwa wakizungumza kwa lugha ya kienyeji ya Runyankole, kulingana na vyanzo vya usalama, tovuti ya habari ya Uganda Radio Network inayomilikiwa kibinafsi iliripoti.

Washiriki wa bendi hiyo wanadaiwa kusema "Rutabandana Waturusya Rugahamuzindaro", ambayo tafsiri yake ni "spika, tumechoka, acha kipaza sauti", iliongeza ripoti hiyo.

Wanamuziki hao wanaripotiwa kuzuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kampala.

Wameshtakiwa kwa kumtusi rais, kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na vyombo vya habari vya ndani.

Si bendi wala polisi wametoa maoni yao kuhusu suala hilo.

Chanzo: Bbc