Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamorocco wanalala mtaani baada ya tetemeko la ardhi kuua watu 2,000

Wamorocco Wanalala Mtaani Baada Ya Tetemeko La Ardhi Kuua Watu 2,000 Wamorocco wanalala mtaani baada ya tetemeko la ardhi kuua watu 2,000

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Huko Marrakesh, maelfu ya watu wamekuwa wakitumia usiku wa pili kwenye maeneo ya wazi kulala. Maeneo ya mapumziko, maeneo ya kuegesha magari na viwanja vya umma vimejazwa na idadi kubwa ya watu wa kila rika wakijilaza kwenye mablanketi. Wachache wanaonekana kulala, wengi wako macho wakitafakari na kuhuzunika.

Kuwa katika usalama wa kiasi wa nje hakuondoi hofu ya kile ambacho tetemeko lingine linaweza kutokea.

Kuna vifusi katika mitaa mingi ya jiji hili la kihistoria la Marrakesh ingawa jiji hilo limekuwa na haueni kuliko maeneo ya milimani kusini-magharibi.

Mmiliki wa mgahawa, Safa El Hakym, anajaribu kukubaliana na kilichotokea. "Asante Mungu ni kuta na vifaa ambavyo vimepotea," anasema. "Mambo muhimu zaidi hayapotei. "Na tunamshukuru Mungu tuna nguvu ya ubinadamu nchini Morocco: sote tuko pamoja na kuweka mioyo yetu katika hili na kusaidiana."

Chanzo: Bbc