Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamalawi kufanya maombi siku 3

9c30cacb548e919375c757e97a282b39.jpeg Rais Chakwera - Malawi

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera (pichani), ameagiza Wamalawi kufunga na kusali kwa siku tatu dhidi ya kuenea kwa virusi vya corona Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Gospel Kazako, Rais Chakwera ameagiza wananchi wote wa Malawi kufunga kwa siku tatu kuanzia Alhamisi.

Pia, Rais Chakwera alitangaza kuwa Jumapili ijayo, itakuwa siku ya kitaifa ya kumshukuru Mungu.

“Rais anaomba yafanyike maombi kwa ajili ya kuwaombea uponyaji wote walioambukizwa na virusi hivi, kuwaombea wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya virusi hivi na kuwaombea wale wote ambao hawajaambukizwa virusi hivi, ili wasiambukizwe na kukiombea kikosi kazi cha Rais kwenye mapambano dhidi ya Covid-19,” alisema Kazako.

Chakwera ni mchungaji mstaafu wa Kanisa la Assemblies of God. Aliongoza kanisa hilo kwa miaka 24. Amekuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress tangu mwaka 2013.

Alichaguliwa kuwa Rais wa Malawi katika duru ya pili ya uchaguzi, iliyofanyika Juni mwaka huu. Duru ya kwanza ya uchaguzi huo ilifanyika mwezi Mei mwaka jana. Katika duru ya pili, Chakwera al imshinda aliyekuwa Rais Peter Mutharika.

Chanzo: habarileo.co.tz