Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliwezaje kukaa kwenye rada siku 11?

Rada Rada 11.png Waliwezaje kukaa kwenye rada siku 11?

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Picha hii ilisambaa kwa kasi duniani na kushangaza kila aliyeiona kutokana na mazingira iliyozunguka upigwaji wake.

Siku mbili baada ya kuokolewa katika pwani ya kisiwa cha Gran Canaria, wahamiaji wa Nigeria wamefikia lengo lao: kusalia Uhipania walau kwa sasa.

Meli ya mafuta ya Alithini II hatimaye imepata idhini ya kutia nanga bila wao kama ilivyobaini BBC Mundo.

Awali ujumbe wa serikali katika kisiwa cha Canary ulikuwa umeripoti kwamba wahamiaji hao watatu watarudishwa kwenye meli mara watakapookolewa.

"Hawa ni Wanigeria watatu walio katika umri halali. Watatu hao wameomba hifadhi na mmoja bado amelazwa hospitalini," waliambia BBC Mundo kutoka kwa wajumbe wa Serikali huko Las Palmas de Gran Canaria. "Meli inaweza kuendelea na mwendo wake bila wao," waliongeza.

Kwa njia hii, hatimaye serikali ya Uhispania ilitoa ruhusa kwa meli kuondoka bandarini, ikiwaacha wahamiaji watatu kwenye kisiwa cha Gran Canaria.

Habari hii pia ilithibitishwa kwa BBC Mundo na shirika lisilo la kiserikali la Caminando Fronteras, ambalo lilikuwa limetaka mamlaka kusimamisha kurejeshwa kwa wahamiaji hao watatu wa Nigeria.

"Ukweli wa kupitia safari ya hatari kama hiyo inapaswa kuzingatiwa kama dalili ya kuchambua kibinafsi hali ya kibinafsi ya wahasiriwa watatu," ilidai NGO, ambayo ilikuwa imeonya kwamba wawili kati ya wahamiaji hao walikuwa wamehamishwa kurudi kwenye meli siku ya Jumanne.

Vile vile, walikuwa wameomba kukaribishwa katika mojawapo ya vituo vya wahamiaji "ili wapate usaidizi unaohitajika wa kutulia kiakili na kisaikolojia kwa kuzingatia hali ya matukio na safari ya hatari ambayo inaweza kuwa mbaya." Ni nini kinachojulikana kuhusu safari hiyo?

Jinsi walivyofikia rada ya usukani haijulikani. Kinachojulikana ni kwamba Wanigeria hao watatu waliabiri meli hiyo k katika bandari ya Lagos, Nigeria, kabla ya Alithini II yenye bendera ya Malta kuanza safari mnamo Novemba 17.

Safari ya kuelekea kisiwa cha Gran Canaria ilidumu kwa siku 11 mfululizo.

Mnamo Jumatatu, Novemba 28, Salvamento Marítimo aliwaokoa baada ya kufaulu kufika Las Palmas, baada ya kuonekana katika sehemu ya chini ya meli.

Mahali walipopatikana ni nafasi iliyoko kwenye kile kiitwacho rada au usukani ya nje ya sehemu ya meli, ambayo huwa wazi na inaweza kushambuliwa na pigo lolote kutoka baharini.

Picha iliyosambaa kwa kasi duniani ilipigwa na mlinzi wa chombo cha uokozi ya Salvamar Nunki, Orlando Ramos Alayón, ambaye aliwaokoa.

Ni jambo la kawaida kunakili shughuli ya uokoaji, alielezea kutoka kwa chombo chao cha Uokoaji wa Bahari.

"Ni kawaida. Huwa tunachukua picha hizo ili kuzihifadhi kama kumbukumbu," Orlando Ramos anaeleza katika taarifa rasmi iliyotolewa siku ya Jumatano. "Kazi halisi, ambayo ni muhimu ni kuokoa maisha ya watatu hao, na wengine ambao hufika uhamishoni bila nguvu, wakiwa wadhaifu, na kuathiriwana baridi kali." Meli

Walikuwa katika hali gani walipofika?

"Kulikuwa na wanaume 3 kutoka kusini mwa jangwa la Sahara waliokuwa wadhaifu baada ya kuathiriwa na baridi kali.

Watu wawili kati ya waliookolewa walipelekwa katika Hospitali ya Doctor Negrin na yule aliyekuwa katika hali mbaya zaidi alisafirishwa hadi Hospitali ya Insular," waliambia BBC Mundo kutoka Salvamento Marítimo

Wawili kati yao waliachiliwa muda mfupi baadaye na kurudishwa kwenye meli ya mwanzoni, lakini baadaye walitolewa tena kwenye meli hiyo baada ya kuomba hifadhi.

Mwathiriwa wa tatu bado amelazwa hospitalini ambako anaendelea kupata matibabu kutokana na upungufu wa maji mwilini, maisha yake hayako tena hatarini, kulingana na mamlaka.

 "Ni sehemu ambayo mtu hawezi kukakaa, ukizingatia hali ya mazingira ya bahari kuu mtu anaweza kufa kutokana na upungufu wa maji mwilini, kuanguka ndani ya maji kutokana na dhoruba ya bahari, na upepo mkali unaosababisha hypothermia ... ni hatari kubwa. Eneo hilo linaweza kujaa maji. Kuna uwezekano mkubwa wa hili kutokea, "alisema Sofía Hernández, mkuu wa Kituo cha Kuratibu Uokoaji cha Las Palmas, ambacho kilielekeza uokoaji wa watu hao watatu, katika taarifa zilizokusanywa na shirika la habari la EFE.

 Ni mara ngapi wahamiaji hufika

Kufikia sasa, mamlaka inayosimamia uokoaji imerekodi visa vingine vitano kama hivyo katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo Januari 2018, Salvamar Nunki iliokoa watu wanne kwenye meli ya Green Sky waliokuwa wamejificha kwenye rada.

Mnamo Oktoba 2020, stowaways wanne walipatikana kwenye gurudumu la meli ya mafuta ya Norway ya Champion Pula, baada ya kusafiri kutoka Lagos hadi Las Palmas.

Mwezi huo huo, Salvamar Nunki iliokoa stowaways 7 kwenye rada ya meli ya Andromeda.

Mwezi mmoja baada ya operesheni hiyo, mnamo Novemba, mashua hiyo hiyo iliokoa mtu aliyekuwa amejificha kwenye rada.

Katika miezi sita ya kwanza ya 2022, shirika lisilokuwa la kiserikali la Caminando Fronteras lilisajili vifo 800 kwenye njia hii.

 Mwaka 2021, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), vifo 1,532 vilirekodiwa kwenye njia hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live