Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliozama wapatika, wengine watatu wafukiwa mgodini

Ajali Mtoo.png Waliozama wapatika, wengine watatu wafukiwa mgodini

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya watu wawili iliyokua ikitafutwa katika mto Gwaseni huko Bamba eneo bunge la Ganze Nchini Kenya, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji imepatikana hii leo.

Afisa wa majanga kaunti ya Kilifi Japheth Chengo, amesema juhudi za idara ya majanga na kitengo cha moto zimefanikisha zoezi hilo, ambalo limechukua siku moja huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Kupatikana kwa miili hiyo, kunafanya idadi ya watu waliofariki katika tukio hilo kufikia watu wanne ambapo awali miili miwili iliopolewa katika mto huo.

Taarifa hizo zinakuja huku ikisemekana Watu wengine watatu wanahofiwa wamefariki kwenye mgodi eneo la Kamtonga – Mwatate, baada ya mgodi kuporomoka kutokana mvua kubwa inayoendelea kunyesha huku juhudi za kuiopoa miili hiyo zikiendelezwa na wachimbaji wa madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live