Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliouawa kambi ya wakimbizi DRC wazikwa

Mweh Ls Waliouawa kambi ya wakimbizi DRC wazikwa

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefanya mazishi ya miili ya watu waliouawa kwenye mashambulizi yalitokea Mei 03, 2024 katika makambi ya wakimbizi mjini Goma.

Imekuwa ni siku yenye shughuli nyingi sana mjini Goma, ambapo shughuli zilibaki zimesimama katika nusu ya mji. Mji wote ulikuwa umeshiriki kwa ajili ya kutoa heshima kwa watu hao waliouawa kikatili na mabomu ya uasi wa M23.

DW imeripoti kuwa, Wakati miili ya waathirika ilipokuwa ikipangwa kwa ajili ya shughuli za heshima, waandamanaji wa harakati za raia walitumia fursa hiyo kufanya maandamano ya hasira mbele ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya Goma, ambapo sehemu ya waathirika walikuwa wamehifadhiwa.

Dav Sikiliza, ni mwanaharakati wa harakati za raia mjini Goma.

"Ni hali ya kukata tamaa kuhusiana na yote yanayotokea. Tunaiomba serikali kuu kulinda raia na kuacha mikakati ya kujihami. Tunapaswa kuchukua hatua ya kushambulia. Ni wakati wa kujibu."

Hii ilifuatiwa na shughuli ya heshima kwa waathirika katika uwanja wa Umoja wa Goma, kwa uwepo wa ujumbe mkubwa uliokuja kutoka Kinshasa, ukiwa na viongozi wakuu sana wa serikali kuu ikiwa ni pamoja na msemaji wa serikali, mawaziri wa haki za binadamu na masuala ya kijamii, na wabunge wa kitaifa. Katika hotuba yake, Waziri wa kitaifa wa masauala ya kijamii amesema, Modeste Mutinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live