Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliotorokea Afrika Kusini warudishwa nchini

Johannesburg South Africa Worship Impartation Service Waliotorokea Afrika Kusini warudishwa nchini

Tue, 7 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WATANZANIA 100 waliondoka nchini kinyume na sheria na kutokomea Afrika Kusini, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kuondoka nchini bila kufuata taratibu za uhamiaji.

Watuhumiwa hao ambao wengi wao wameonekana kuwa ni vijana, wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na wote wamekiri kutenda kosa hilo na wameiomba mahakama iwasamehe.

Hata hivyo, Hakimu Simba alisema kuwa haoni faida yoyote ya kuwapeleka watuhumiwa hao gerezani, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa corona.

“Sioni faida yoyote ya kuwapeleka gerezani, lakini mahakama inawapa onyo kali na inawaachia kwa masharti msirudie kutenda kosa hili kwa miezi sita,” alisema Hakimu Simba.

Awali wakisomewa shtaka lao na wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji. Godfrey Ngwijo, inadaiwa Julai 3, 2020 huko katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, washtakiwa wote 100 walikutwa wakiwa wameondoka nchini kinyume na sheria bila kufuata utaratibu wa kutoka na kuelekea Afrika Kusini.

Wakisomewa maelezo ya awali imedaiwa katika tarehe zisizojulikana washtakiwa hao waliondoka nchini bila kufuata utaratibu na kwamba Julai 3, mwaka huu walirudishwa nchini baada ya uchunguzi na kugundulika kuwa ni wahamiaji haramu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live