Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliotengana na familia zao wafunguka mazito

SouthSudan Uganda UNHCR RF2 2 1024x640 Waliotengana na familia zao wafunguka mazito

Sun, 4 Sep 2022 Chanzo: dar24.com

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la kuratibu misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Kusini, Sara Beysolow Nyanti awatembelea waathirika wa machafuko ya Adediang na Malakal katika jimbo la Upper Nile State na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Waathirika hao, wamesema katika kitongoji cha Tonga mapigano makali yalizuka baina ya vikundi vyenye silaha maeneo jiraji ya kaunti ya Panyikang na kuwalazimisha maelfu ya watu wasiojiweza wengi wakiwa wanawake, wazee na watoto kusaka usalama.

Beyssolow Nyati, akiambatana na ujumbe wake wa mamlaka ya eneo hilo, pia wamezungumza na jamii zinazowahifadhi waathiriwa hao ambao ni wanawake, wazee na vijana na walipata fursa ya kusimulia changamoto za kukimbia usiku wa manane na kutenganishwa na familia zao.

Bi.Sara amesema, “Tunaweza kufanya kitu kwa wale waliotenganishwa na wapendwa wao wanaoishi sehemu nyingine, tutajaribu kadri tuwezavyo, tuko na wenzetu ambao wanafanyakazi kwa pamoja ili kuangalia jinsi gani tunaweza kuanza kuwafuatilia watoto na kuwaunganisha tena na mama zao.

Ameongeza kuwa, “Hata kuna watoto wengine wapo hapa na wazazi wao hawapo, hivyo tunajaribu kutafuta wazazi wa watoto hawa. Na watu wote hawa mnaowaona wanajaribu kupata msaada wa kuwasaidia.”

Wadau wa misaada ya kibinadamu wanajaribu kwa kila hali kukusanya rasilimali fedha na watu, ili kukabiliana na mahitaji ya dharura yanayohitajika haraka kama vile malazi, maji, huduma za usaji na kujisafi, ulinzi, huduma za afya, chakula na lishe.

Chanzo: dar24.com