Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliopotosha ujumbe uliotolewa na Kenya waonywa

DAMS1 1 660x400 Waliopotosha ujumbe uliotolewa na Kenya waonywa

Thu, 30 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  Damas Ndumbaro, amewataka Watanzania kuisemea nchi mazuri ili kuwa na diplomasia nzuri na Mataifa mengine na kuachana na upotoshaji unaoenezwa mitandaoni hasa baada ya ujumbe wa Kenya uliokuwa ushiriki katika maziko ya Kitaifa kushindwa kufika.

Ndumbaro ameyasema kufuatia kuenea taarifa za uzushi katika mitandao ya kijamii, hususani baada ya ujumbe uliokuwa uiwakilishe Kenya katika hafla ya Kitaifa ya kuaga mwili wa Hayati Benjamin Mkapa, iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru siku ya Julai 28, 2020, kushindwa kutua nchini kutokana na hitilafu za kiufundi.

“Ndege hiyo ya Kenya ilishindwa kutua Tanzania kutokana na hitilafu za kiufundi, ambazo ziligundulika na Rubani muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Nairobi, kwenye mitandao watu wanahusisha hilo na COVID-19 na mambo mengine”  Ndumbaro.

“Niwaambie Watanzania tuna muda mchache sana ambao tunapaswa kuutumia kufanya mambo ya maana na kimaendeleo siyo kukaa mitandaoni kusuka maneno ya uongo, fitina na ugombanishi, niwasihi Watanzania watumie vizuri muda wa mitandaoni kwa sababu wanayoyafanya ni uhalifu” Ndumbaro

MAGUFULI AWAACHA HOI VIONGOZI MSIBANI WAKIWA NA MAJONZI KUHUSU ATAKAPOZIKWA MWINYI

Chanzo: millardayo.com