Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliopata chanjo ya COVID-19 Afrika wamefikia milioni 75

Chanjo  Ed Idadi ya watu waliopata chanjo ya COVID-19 Afrika imefikia milioni 75

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hadi kufikia September 13, imethibitishwa kuwa visa vya Covid-19 kutoka nchi 55 za Afrika vimefikia jumla ya 8,044,725 huu idadi ya watu waliochanjwa barani huku ikiwa imefikia 75,874,065.

Mpaka kufikia sasa watu waliopoteza maisha kwa kesi za Corona imefikia 202,878 na waliopona kutokana na ugonjwa huo ni 7,286,009. Afrika Kusini bado inaongoza kwa idadi kubwa ya visa vya COVID-19 ambapo mpaka sasa ni watu 2,858,195 walioambukizwa na watu 84,877 wamefariki dunini.

Nchi nyingine zenye idadi kubwa ya visa vya Corona ni pamoja na Morocco (Visa 904,647), Tunisia (Visa 685,019), Libya (visa 323,930), Ethiopia (visa 323,104), Egypt (visa 292,957) na Kenya (visa 243,725).

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa AllAfrica ambayo huonesha maambukizi ya kila nchi kutoka Barani Afrika. Takwimu hizi hukusanywa na Kituo cha Sayansi ya Mifumo na Uhandisi (CSSE) kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ambayo huchambua taarifa za COVID-19 kutoka mabara yote pamoja na vyanzo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na taasisi zingine za masuala ya Afya kutoka barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live