Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa mlipuko Somalia wafikia 81

90355 Mlipukopic Waliokufa mlipuko Somalia wafikia 81

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mogadishu.  Idadi ya watu waliokufa mlipuka wa bomu ndani ya gari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu imefikia 81, msemaji wa Serikali ameeleza.

Mlipuko huo uliotokea majira ya asubuhi katika eneo lenye watu wengi, ndilo shambulio kubwa kuwahi kutona katika nchi hiyo ndani ya miaka miwili.

Hadi sasa hakuna kindi lililoeleza kuhusika na shambulio hilo, ingawa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed amekishutumu kikundi cha Al- Shabaab, ambacho mara kwa mara kimekuwa kinafanya mashambulizi ya namna hiyo kwa lengo la kuiangusha Serikali ya Somalia.

“Idadi ya vifo imefikia 81 hadi sasa. Watu wengine wawili wamekufa kutokana na majeraha, amesema Ismail Muktar, msemaji wa Wizara ya Habari ya Somalia.

Moja wa waliokufa baadaye ni mmoja wa majeruhi aliyehamishiwa nchini Uturuki Jumapili kwa kutumia ndege ya kijeshi ya nchi hiyo.

Muktar amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi wakati shughuli za uokoaji zinaingia siku ya tatu.

Zaidi ya watu 20 waliorodheshwa miongoni mwa wasiofahamika mahali walipo baada ya shambulio, lakini 12 kati yao wameonekana, watano wakiwa wamekufa.

Watu 125 walijeruhiwa katika mlipuko huo wa Jumamosi, idadi ambayo imesababisha hali ngumu katika hospitali za Mogadishu.

Miongoni mwa waliokufa ni wanafunzi 16 wa chuo Kikuu cha Banadir waliokuwa wanasafiri katika basi katika eneo la mlipuko huo.

Mlipuko huo ni wa pili kuikumba Somalia baada ya ule wa mwaka 2017 uliotokea karibu na tanki la mafuta na kuua watu zaidi ya 500.

Chanzo: mwananchi.co.tz