Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa katika mlipuko wa bomu Mogadishu wafikia 76

90190 Mlipukopic Waliokufa katika mlipuko wa bomu Mogadishu wafikia 76

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mogadishu. Idadi ya watu waliokufa katika mlipuko wa mabomu yaliyokuwa ndani ya gari leo asubuhi katika kituo kimoja cha ukaguzi chenye shughuli nyingi Mogadishu, Somalia imefikia 76.

Mkuu wa hospitali ya Medina, Mohamed Yusuf amethibitisha idadi hiyo kuwa watu wengine 70 wamejeruhiwa.

Awali, msemaji wa serikali Ismail Mukhtar alinukuliwa akisema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu zaidi ya watu 60 wamekuwa wamepelekwa katika hospitali mbalimbali.

Hilo limekuwa mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kutokea katika siku za karibuni mjini Mogadishu.

Kapteni Mohamed Hussein amesema mlipuko huo ulikilenga kituo cha kukusanya kodi wakati wa pilikapilika za asubuhi wakati wakazi wengi wakiingia kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu aliyehusika na shambulizi hilo.

Kundi la itikadi kali la Al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda mara kwa mara hufanya mashambulizi ya aina hiyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz