Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa Baada Ya Basi Kutumbukia Mtoni Wafika 32

Ajali Mtoni 1 Waliokufa Baada Ya Basi Kutumbukia Mtoni Wafika 32

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliopoteza maisha ya baada ya basi walilokuwa wakisafiria, kusombwa na maji katika Mto Enziu, Ngune, Kaunti ya Kitui nchini Kenya imeongezeka na kufikia 32.

Miili mingine imegunduliwa baada ya juhudi za kulitoa basi hilo katika Mto Enziu kukamilika ambapo kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa Katoliki Kaunti ya Kitui, Bishop Joseph Mwongela, waumini wote wa Kanisa Katoliki, wamearifiwa juu ya kufika na kuitambua miili ya ndugu zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bishop Mwongela amesema kanisa limepata pigo kubwa kwa kupoteza waumini wake na kueleza kuwa, kati ya waliofariki, kulikuwa na waumini wawili wa dini ya Kiislamu ambao tayari miili yao imezikwa na kwamba mipango ya mazishi ya waumini wa kanisa hilo, inaendelea.

Katika ajali hiyo iliyotokea Jumamosi ya Desemba 4, majira ya saa tano asubuhi, basi ambalo ni mali ya Shule ya Seminari ya St. Joseph Mwingi iliyopo chini ya Kanisa Katoliki, lililokuwa limebeba zaidi ya watu 32, wengi wakiwa ni wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mwingi, lilisombwa na maji katika Daraja la Mto Enziu na kusababisha maafa hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live