Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliohudhuria sherehe za madaraka watakiwa kupimwa Covid-19 na kuingia Karantini

Cb66d0d504436391 Waliohudhuria sherehe za madaraka watakiwa kupimwa Covid-19 na kuingia Karantini

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kisumu imekuwa ikirekodi idadi ya juu ya maambukizi ya maradhi ya Covid-19 na kuna wasiwasi kuhusu hali ilivyokuwa wakati wa Madaraka Dei

- Waliohudhuria wametakiwa kupimwa na kuingia karantini kama nji moja ya kuhakikisha maambukizi hayajaenea

- Wakazi walionekana huku wakipuuza sheria za kukabiliana na maradhi hayo kama vile kukosa kuvalia maski

- Tayari naibu gavana wa Nyeri ameingia karantini na kupimwa virusi vya Covid-19 baada ya kuhudhuria sherehe hiyo Juni 1

Waliohudhuria sherehe za Madaraka Dei juni 1 Kisumu wametakiwa kupimwa maradhi ya Covid-19 na waingie karantini.

Naibu gavana wa Nyeri Dkt Caroline Karugu aliwataka wote waliohudhiria sherehe hiyo kufanya hivyo kutokana na kuongezeka kwa maambukizi Kisumu.

"Huku Kisumu ikirekodi idadi ya juu ya Covid-19. Sisi ambao tulizuru humo tunafaa kuingia karantini na pia tupimwe. Mimi hufanya kazi na watu ambao hali yao kiafya si nzuri na kwa sababu ya upendo wangu kwao, naingia karantini," alisema Karugu.

Wito wa mwanasiasa huyo ni kwa viongozi wenzake akisema hiyo ndiyo hali ya kuwajibika katika jamii.



Karugu alishukuru Mungu baada ya matokeo kuonyesha kuwa hakuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Alisema amekuwa na bahati kwani licha ya kuvunja baadhi ya sheria zilizowekwa kukabili janga hilo angali hajaambukizwa.

Kisumu Alhamisi ilirekodi idadi ya juu zaidi nchini ya virusi hivyo na kuchangia asilimia 30 ya maambukizi yote nchini.

Kulikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi serikali itaweza kuhakikisha sheria za Covid-19 zinafuatwa kwenye sherehe hizo za madaraka.

Ilikuwa wazi baadaye kuwa haikuweza kufanya hivyo kwani wakazi walionekana wamekongamana haswa eneo la Kondele ambapo hawakuvalia maski.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke