Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki mlipuko wa Gesi Nairobi wafikia 6

Gesi Embakasi Waliofariki mlipuko wa Gesi Nairobi wafikia 6

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu zaidi wamefariki dunia kutokana na majeraha waliyoyapata wakati wa mlipuko wa gesi ya Embakasi, na kufanya idadi ya watu waliofariki dunia kufikia sita kufikia sasa kutokana na tukio hilo.

Taarifa ya Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura inaeleza kuwa watu wengine saba wako katika hali mahututi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) na Hospitali ya Kufundisha, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH).

Hospitali ya KNH ilipokea wagonjwa 67 wa tukio hilo, huku sita wakiwa katika hali mbaya huku KUTRRH ikishuhudia jumla ya wagonjwa 27, wanane wakiwa tayari wameruhusiwa na 19 wapo chini ya uangalizi, wakiwemo wanaume 10, wanawake sita na watoto wadogo watatu.

Miongoni mwao, mgonjwa mmoja yuko katika hali mbaya kutokana na kuungua sana na majeraha ya kuvuta pumzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live