Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki kwa maporomoko ya taka Kiteezi wafikia 25

Vifo Google Waliofariki kwa maporomoko ya taka Kiteezi wafikia 25

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko katika fampo la taka jijini Kampala imefikia watu 25, huku matumaini ya kuwapata manusura zaidi yakiendelea kufifia.

Tukio hilo, lilitokea Agosti 10, 2024 katika Wilaya ya Kiteezi iliyopo Kaskazini mwa jiji kuu la Kampala, baada ya kuanza kwa maporomoko ya ardhi yaliyosabajishwa na Mvua katika eneo la kutupia taka.

Waziri wa majanga nchini Uganda, Lillian Aber amesema hadi kufikia Jumatatu jioni (Agosti 12, 2024), miili 25 ilikuwa imepatikana na hakukuwa na manusura.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Mvua kubwa zikizonyesha zimeathiri shughuli za kupata miili zaidi, huku Rais Yoweri Museveni akiliagiza Jeshi kutoa usaidizi katika zoezi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: