Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliochanjwa kuruhusiwa kwenye mikusanyiko Rwanda

Rwadan Rwanda

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Rwanda imeanza kulegeza masharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kuruhusu shughuli za kijamii pamoja na kumbi za starehe kufunguliwa .

Aidha serikali hiyo imetoa agizo kuwa watakaoruhusiwa kushiriki kwenye sehemu za mikusanyiko kama sherehe na maonesho ni watu waliopata chanjo ya Corona pekee.

Agizo hilo litaanza kutekelezwa Septemba 23. Hata hivyo Rwanda imefika hatua hiyo baada ya idadi ya maabukizi kushuka kwanzia mwezi Agosti mwaka huu.

Shirilika la Afya Dunia WHO , linaendela kuwasisitiza watu wajitokeze kupata chanjo ya Corona wahimarishe kinga ya mwili na kupunguza maambukizi kusamba kwa kasi na kusababisha idadi kubwa ya vifo Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live