Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walioambukizwa corona Kenya wafikia 225, vifo 10

102628 Pic+kenya+corona Walioambukizwa corona Kenya wafikia 225, vifo 10

Wed, 15 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka mpaka kufikia wagonjwa 225 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wapya tisa.

Waziri wa Afya, Mutahi Kabwe amesema sampuli 803 zilichukuliwa na kupimwa tangu jana Jumanne Aprili 14, 2020 ambapo serikali iliripoti maambukizi 216 tangu virusi vya corona vilipothibitishwa kwa mara ya kwanza nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la Daily Nation, Waziri Kagwe amesema wagonjwa wote ni raia wa Kenya na maambukizi matano yamepatikana Nairobi na mengine manne yamepatikana Mombasa.

Amesema jumla ya watu 2,366 wamepimwa na kati yao 1,911 wameruhusiwa huku wengine 455 wakiendelea kuangaliwa.

Amesema wagonjwa wengine 12 wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona ugonjwa huo na kufanya idadi ya waliopona kufikia 53.

Pia, waziri huyo ameripoti kifo cha mtu mmoja na kufanya idadi ya vifo nchini Kenya kufikia 10 tangu ugonjwa huo ulipotangazwa.

Pia Soma

Advertisement
Wakati akisema Kenya haiko kwenye hatari, Waziri Kagwe ameitaka jamii kuchukua hahadhari ana kufuata miongozo inayotolewa na serikali ili kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Amesema ili kuvishinda virusi hivyo hawana budi kupima watu wengi, kujitenga na mikusanyiko na kupata matibabu kwa walioambukizwa.

“Watakaoishinda vita hii siyo serikali bali ni Wakenya kwa kuleta ushirikiano,” amesema Waziri Kagwe.

Awali wizara ya afya ilibainisha kwamba upimaji wa watu wengi utakuwa kipaumbele chao na vifaa vya kupimia zaidi ya 12,000 vitasambazwa nchi nzima.

Wizara hiyo ilibainisha kwamba maeneo ya kipaumbele ni vituo vya karantini, mabweni, sehemu za kujitenga, hospitali na maeneo yenye watu wengi kama vile Kibra, Nairobi na maeneo ya kaunti za Mandera na Siaya.

Kagwe ametangaza kwamba timu maalumu inayoongozwa na Dk Patrick Amoth ambaye ni kaimu mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya, imekwenda Siaya.

Amesema timu hiyo itatathmini hali ya karantini na maeneo ya kujitenga katika kaunti hiyo na kuwashirikisha wananchi ili wote wawe katika mwelekeo mmoja. Ameongeza kuwa vifaa kwa ajili ya kujikinga vimetumwa katika kaunti hiyo.

Mpaka sasa, zaidi ya watu milioni 2 wameambukizwa virusi vya corona ulimwenguni kote tangu virusi hivyo viliporipotiwa kwa mara ya kwanza huko Wuhan, China Desemba 31, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz