Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wapata makaburi ya halaiki mashariki mwa Congo

C618950d F355 4657 94e9 192fbe48e10f Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wapata makaburi ya halaiki mashariki mwa Congo

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekuta makumi ya maiti kwenye makaburi ya halaiki.

Ugunduzi huo umekuja baada ya msururu wa mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo la Ituri.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, alisema miili ya watu 42 wakiwemo wanawake na watoto imegunduliwa katika kijiji cha Nyamamba, na wanaume wengine saba katika kijiji cha Mbogi.

Walinda amani hao walikuwa wameanzisha doria katika eneo hilo baada ya ripoti za mashambulizi ya wanamgambo wa Codeco.

Wapiganaji wake hasa wanatoka katika jamii ya wakulima ya Lendu ambayo kwa muda mrefu imekuwa katika mgogoro na wafugaji wa Hema.

Chanzo: Bbc