Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walinda amani UN wasimamishwa madai ya unyanyasaji wa kingono DR Congo

Walinda Amani UN Wasimamishwa Madai Ya Unyanyasaji Wa Kingono DR Congo Walinda amani UN wasimamishwa madai ya unyanyasaji wa kingono DR Congo

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasema kuwa umewasimamisha kazi baadhi ya walinda amani wake kutokana na ripoti za utovu wa nidhamu.

Ilisema ina sera ya kutovumilia kabisa unyonyaji na unyanyasaji wa kingono.

Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa shutuma hizo ni dhidi ya walinda amani wanane wa Afrika Kusini.

Ujumbe wa Monusco umekabiliwa na shutuma za hapo awali za unyanyasaji wa kijinsia.

Ina zaidi ya wanajeshi 14,000 mashariki mwa DR Congo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na maandamano kadhaa dhidi ya Umoja wa Mataifa ambayo inashutumiwa kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya makundi yenye silaha.

Chanzo: Bbc