Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu waomba serikali iwape bunduki

BUNDUKI Kujiuaaa Walimu waomba serikali iwape bunduki

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muungano wa Walimu wa Elimu ya Msingi nchini Kenya (KUPPET) umeitaka serikali kutoa mafunzo ya kijeshi kwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo yasiyo salama kote nchini na kuwapa bunduki ili kuimarisha usalama wao.

Wakizungumza mjini Isiolo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka huu, maafisa wa KUPPET na walimu kutoka kaunti ya Isiolo wanasema kuwa walimu wanaendelea kuhangaishwa na kutishwa na Tume ya Utumishi wa Walimu kuendelea kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

Edward Obwocha ambaye ni Katibu wa Taifa wa chama hicho amewataka walimu hao kutoa wito wa kutolewa kwa bunduki na walimu walikubaliana kwa pamoja.

Hivi karibuni ya Tume ya Utumishi wa Walimu aliwashtaki walimu waliotoroka kutoka maeneo ya Kaskazini mwa Kenya ambako maisha yao yalikuwa hatarini ambapo walimu hao wanasema ni kinyume na utaratibu kwa kuwa walikimbia ili kulinda maisha yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live