Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu, wanafunzi ruksa kutumia usafiri wa umma

MUSEVENI Walimu, wanafunzi ruksa kutumia usafiri wa umma

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni (pichani) ameruhusu walimu na wanafunzi kutumia usafi ri wa umma huku wakichukua tahadhari zilizotolewa za kujikinga na virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (Covid-19).

Kauli hiyo ya Rais Museveni imekuja baada ya hivi karibuni Wizara ya Elimu na Michezo kupiga marufuku walimu na wanafunzi kutumia usafiri wa umma zikiwemo teksi, daladala na pikipiki maarufu bodaboda wakati shule zitakapofunguliwa Oktoba 15 mwaka huu kwa wanafunzi wanaomaliza masomo na wenye mitihani.

Wizara iliwashauri wazazi ambao hawana magari binafsi kuwaandikisha watoto wao katika shule za jirani na nyumbani kwao ili kupunguza hatari za kiafya, kuepuka gharama zisizo za lazima na usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwenda shule, pia hata magari ya shule yalitakiwa yasisafiri umbali wa zaidi ya kilometa tano.

Kutokana na hali hiyo, Museveni aliamua kutoa uamuzi tofauti kwa kusema kuwa ikiwa taratibu zilizowekwa kwenye jamii, usafiri wa umma na shule zitazingatiwa, hakuna sababu ya kuwazuia walimu na wanafunzi wasitumie usafiri wa umma.

“Hata ninyi walimu, wakati mnakuja kutoka katika makazi yenu, msikubali kupanda gari ambalo limejaa, na kama watakuwa wanawapa shida, fikirini namna ya kufanya kwa sababu haya ni madarasa ya watahiniwa tu siyo shule nzima, mnaweza kuweka kambi karibu na shule kwa sababu baadhi ya majengo ya shule yako wazi,”alisema Museveni.

Aliwataka walimu wanaohofia kwenda na kurudi nyumbani kutumia vyumba vya madarasa kulala ili waweze kuwafundisha watoto.

Chanzo: habarileo.co.tz