Mama mmoja nchini Nigeria amewashutumu walimu wa mwanawe kwa kula chakula cha mtoto wake.
Mwanamke huyo alisema kila mara alishuku kuwa kuna mtu alikuwa akila chakula cha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambaye huwa anabeba chupa iliyojaa mlo.
Akijua kuwa mwanawe hali ndizi za kuchemsha, alimpakia kwa haraka kwenye chupa (Container) ya kubeba chakula na kumpeleka shuleni. Cha kushangaza, bado alirejea nyumbani na chupa tupu.
“Nilimpa ndizi mbichi zilizochemshwa na mchuzi wa mboga! Nikijua vizuri mwanangu anachukia ndizi mbichi. Nilishtuka aliporejea nyumbani na chupa tupu. Kwa hivyo ulikuwa mtihani, kwa sababu chupa yake ni kubwa na kwa mtoto wa miaka 2 hawezi kula sana.
Nilijua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa! Angalau anapaswa kurejea nyumbani na chakula alichobakisha, ilibidi nitumie ujanja ndipo nijue kile kilikuwa kinaendelea na sasa majibu nimepata bayana. Hapo ndipo nilijua walimu wake wanakula vizuri.”