Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu 1,566 wafanya kazi bila nyaraka za ajira kisheria

36479e9ba7a2e168b93c281bd8601d9e Walimu 1,566 wafanya kazi bila nyaraka za ajira kisheria

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RIPOTI ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019/2020 imebainisha kuwa walimu 1,566 katika shule za serikali wanafanya kazi bila kuwa nyaraka za ajira kisheria.

Ripoti iliyowasilishwa katika bunge la seneti, imeonesha kuwa walimu ambao ni asilimia 6.6 ya walimu wote nchini wanafanya kazi bila kuwa na mafaili kutokana na uzembe wa wakaguzi wa ndani.

Imebainika kuwa walimu 23,617 katika wilaya 11 hawana taarifa zinazoonesha jinsi walimu 4,087 waliajiriwa, hawana barua za ajira.

Ripoti ilibainisha kuwa walimu 762 wanafanya kazi bila ya kuwasilisha vyeti vya shule hivyo kusababisha sintofahamu iwapo wanakidhi vigezo vya kufanya kazi katika maeneo waliyopo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Elimu Rwanda, Irenée Ndayambaje alibainisha kuwa idadi ya walimu wasio na sifa wataachishwa kazi ili kupisha nafasi ya walimu takribani 7,214 wamepanga kuajiriwa mwaka huu.

“Tunaandaa orodha ya watu wasio na sifa na kuwasilisha wizara ya elimu, ili wasiotaka kujiendeleza kuacha kazi,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz