Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu 1,038 wapata ajira Kigali

Ed53dd07865a218c889aae20ec020b7a Walimu 1,038 wapata ajira Kigali

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Kazi na Huduma kwa Umma (MIFOTRA) imeajiri walimu 1,038 baada ya kufaulu mitihani waliyofanya mwaka jana.

Aidha, serikali inaendelea kuajiri walimu 29,000 wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (TVET).

Takwimu hizo ni walimu 7,214 waliokadiriwa awali kuajiriwa na Bodi ya Elimu Rwanda katika mkakati wa kuboresha uwiano kati ya walimu na wanafunzi kwa wanafunzi 59 kwa mwalimu mmoja shule ya msingi na wanafunzi 29 kwa mwalimu mmoja kwa sekondari.

Mkurugenzi Mkuu wa REB, Dk Irenee Ndayambaje aliliambia gazeti la New Times kuwa mchakato wa ajira kwa walimu unaenda taratibu kutokana na ugonjwa wa corona. Alisema kutokana na ugonjwa huo, wameweka vituo viwili vya kutoa ajira katika kila wilaya ili kukabiliana msongamano wa watu kila chumba kinahudumia waombaji 15 pekee.

Alisema kipindi hiki, idadi kubwa ya walimu wamefika kuomba ajira katika wakati huu ambao serikali inatarajia kudahili idadi kubwa ya wanafunzi katika mwaka ujao wa masomo.

“Serikali inajenga madarasa mapya kwa matarajio ya kudahili watoto wapya Septemba mwaka huu, hivyo walimu hawa wanasubiri orodha itakayowekwa shule nyingi,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz